TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, July 28, 2009

Kiwanda cha kuchambulia pamba chateketea

11:00 AM

Zaidi cha kilo milioni 1.6 za pamba safi zenye thamani ya Sh. Mililioni 726 zimeteketea kwa moto baada kiwanda cha kuchambua pamba cha Afrissian kilichopo katika kijiji cha Sanga wilayani Kwimba mkoani hapa kuteketea kwa moto.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Elias Kapinga, alisema kiwanda hicho kinamilikiwa na mfanyabiashara Ally Abush, mkazi wa mjini Shinyanga.

Alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, saa 11:00 alfajiri wakati maghala makubwa mawili na madogo yenye pamba safi kilo 1,650,000 yalipoteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana.

Katika tukio hilo, wafanyakazi wawili wa kiwanda hicho, Andani ambaye ni meneja na Shinje Deus ambaye ni afisa ununuzi wa kiwanda walijeruhiwa baada ya kukatwa na mabati mapajani na usoni katika harakati za kujiokoa.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA