TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, July 16, 2009

Hivi ndivyo alivyotufanyia askari wa usalama barabarani

12:33 AM

http://tzlivenews.com/images/com_adsmanager/ads/22a.jpg

Mtoto huyu George Gabrieli(14) wa darasa la tano shule ya msingi Mpanda alikuwa akifua nguo za shule mtoni kando ya daraja la mto misunkumilo barabara iendayo kigoma tokea mpanda mjini,
Ilikuwa siku tulivu ya jumapili tarehe 12/07/2009 baada ya kutoka kanisani akijiandaa na usafi wa shule siku inayofuata yaani jumatatu,alipopatwa na ajali iliyosababishwa na uzembe wa askari wa Trafic,akieleza ilivyotokea ajari hiyo Binti Stumai aliyekuwa akifua na mtoto huyo anasema askari huyo wa traffic alisimamisha gari hiyo kama kawaida ya askari hao na baada ya ukaguzi na mabishano ya hapa na pale kati ya askari na dreva wa gari hiyo hatimae askari alimuamuru dreva wa gari hiyo aingie ndani ya gari waelekee kituo cha polisi na zaidi ya hayo alimuamuru pia ampatie funguo za gari ili aendeshe yeye gari hiyo,kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo

http://tzlivenews.com/images/com_adsmanager/ads/22b.jpg
wanasema ni wazi Trafiki huyo hana uzoefu wa kuendesha kwani aliiondoa gari kwa kasi ya mtu ajifunzae na ghafra aliacha njia na kuingia eneo la mto ambako mtoto huyo na wenzake walikua wakifua nguo na bila kutegemea mtoto aligongwa na kuumia vibaya kwa kuchanika kichwa na kuvunjika miguu yote miwili,kama kawaida ya ajali askari huyo mzembe E 1634 PC Omary pamoja na dreva wa gari hiyo No.T 253 AHD walikurupuka wakitaka kukimbia lakini walidhibitiwa na wasamalia wema waliokuwepo eneo la tukio mpaka ulipopatikana msaada wa kumuwahisha mtoto huyo hospitali ya wilaya mpanda,akiongea kwa majonzi makubwa mama wa mtoto huyo Bi.Devota Meza, anasema anasikitishwa sana na uzembe wa askari huyo kwani umesababisha mateso makubwa kwa mtoto wake ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha yake,

Swali la msingi ni je, askari hawa wako barabarani kwa usalama na maslahi ya taifa au wako barabarani kwa maslahi binafsi na kuhatarisha maisha ya wana taifa hili? Na je, sheria inasemaje kuhusu askari kuendesha chombo alichokamata kutokana na kuvunja sheria za barabara?

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA