TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, July 17, 2009

CCM Arusha wadaiwa kuandaa vijana kumng'oa Mbunge Slaa mwakani

2:08 PM
http://www.fahnenversand.de/fotw/images/t/tz%7Dccm.gif
Na Hemed Kivuyo,Arusha

ZAIDI ya vijana 50 kutoka mkoani Arusha, wameandaliwa kupelekwa katika Jimbo la Karatu, katika mkakati wa kumng’oa Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Dk. Willibrod Slaa.Mwananchi limeelezwa.

Habari za uhakika zinasema mpango huo ulioanza mwanzoni mwa Aprili mwaka huu, sasa umekamilika tayari kwa kumng'oa mbunge huyo machachari kupitia Chadema.

Chanzo cha habari hii kilisema CCM imepania kupata ushindi katika jimbo hilo ambalo kwa muda mrefu sasa, limekuwa likishikiliwa na mbunge wa chama cha upinzani na ambaye amekuwa akikisulubu vikali bungeni.

Hivi karibuni chama hicho kilianza kampeni ya kugawa kadi kwa wanachama wapya katika kujizatiti kwa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Ilidaiwa kuwa kikundi cha wazee wa chama hicho ambacho kilipewa jukumu la kufanya ziara za mara kwa mara katika jimbo hilo ndilo lililotoa pendekezo la kuongeza vijana ambao wataweka kambi kwa muda usiojulikana katika jimbo hilo.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA