TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, July 18, 2009

BBC yafichua, nani mmiliki wa Migingo?

1:18 PM
http://www.monitor.co.ug/artman/uploads/1/Migingo-islands-3.jpg
Uchunguzi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ambao ulijumuisha wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa zinazoshughulikia maswala ya kijiografia umedhihirisha kwamba Kenya ndiye mmiliki halisi wa kisiwa cha Migingo ambacho kimezusha mzozana kati yake na nchi jirani ya Uganda.

Sheria ya kikoloni

Ili kutatua mvutano huo, serikali za Kenya na Uganda zimeunda jopo la pamoja la masoroveya kufanya utafiti, kupima na kuweka mipaka ya visiwa vilivyoko kwenye ziwa Viktoria.

Nchi zote mbili zimetoa kitita cha takriban dola za Marekani milioni tano kufanikisha shughuli hiyo.

Lakini baada ya karibu mwezi mmoja wa kuendesha shughuli zake, sintofahamu imelizonga jopo hilo.

Hata hivyo, Idhaa ya Kiswahili ya BBC imekuwa ikifanya utafiti kuthibitisha nani hasa anastahili kumiliki kisiwa hicho kidogo kilichopo Ziwa Victoria.

Tulizungumza na waakilisha wa jopo hilo kutoka pande zote mbili. Bwana Dennis Obo ambaye ni msemaji wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya miji.

Pia tulizungumza na mwenzake kutoka Kenya, Ephantus Murage ambaye ni mkurugenzi wa usoroveya.

Wote walizungumzia umuhimu wa kutafsiri kwa makini sheria ya kikoloni ya mwaka wa 1926 ambayo ilitumiwa kueleza mipaka ya Kenya na Uganda.

Koloni za Uingereza

Sheria hiyo inazingatiwa kuwa amana kubwa ya kufumbua kitendawili cha umiliki wa kisiwa cha Migingo.


Dr Wafula Okumu ni Mkuu wa Mpango wa uchambuzi wa masuala ya usalama wa Afrika katika taasisi ya mafunzo ya usalama Afrika Kusini.

Aliiambia BBC kwamba mipaka ya Kenya na Uganda ilipimwa kwa kuanza na visiwa vilivyoko kwenye ziwa Victoria.

Mkurugenzi wa utafiti katika kitengo kinachoshughulikia maswala ya mipaka kwenye chuo kikuu cha Durham, Uingereza.

Alisema, "ninahisi maelezo ya Uingereza yalikiweka kisiwa upande wa Kenya."

Idhaa ya Kiswahili iliwasiliana pia na serikali ya Marekani kwenye kitengo kinachohusika na uchambuzi wa kijografia na mipaka ya kimataifa.

Umoja wa Mataifa

Kitengo hicho kilituma majibu yake kupitia barua pepe: "Msimamo wa Marekani ni kwamba, kisiwa cha Migingo kama ilivyofafanuliwa kwenye maelezo ya mipaka, katiba na sheria ya kikoloni ya Uingereza ya mwaka wa 1926, kipo nchini Kenya."

Tulitaka pia msaada wa Umoja wa Mataifa. Msemaji wa katibu mkuu wa UN, Yves Sorokobi alisema, "Kwa Umoja wa Mataifa kujihusisha au hata kutoa maelezo yoyote kuhusu kisiwa cha Migingo, serikali husika lazima zitume maombi rasmi kwa UN."

Hata hivyo hakuna nchi yoyote, Kenya au Uganda, ambayo imewasilisha ombi hilo kwa Umoja wa Kimataifa.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA