TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, July 28, 2009

Ban ausihi ulimwengu ujirekibishe kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

3:08 PM
KM Ban Ki-moon, kwenye hotuba alioitoa Ulaanbaatar, mji mkuu wa Mongolia Ijumatatu ya leo, kuhusu "Marekibisho ya Kudhibiti Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani" alieleza kwamba nchi zilizozungukwa na bara husumbuliwa sana na vizingiti vinavyokwamisha juhudi za kusukuma mbele maendeleo yao, hususan katika kipindi ambacho nchi hizi zisio na pwani huwa zinaathirika pia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,
kijumuisha pia taifa analolizuru la Mongolia, ambapo tatizo la kuenea kwa jangwa huko ni moja ya suala kuu linalozikaba nchi kama hizi kimaendeleo, hali ambayo hunyima umma fursa ya kupata riziki. Uharibifu wa maeneo ya malisho ya wanyama, au machungani, katika Mongolia, aliongeza kusema KM, huathiri sana uchumi wa taifa, na vile vile kuharibu mila na utamaduni wao. Watu wa Mongolia, alitanabahisha KM, ni miongoni mwa watu bilioni 2 ulimwenguni - sawa na thuluthi moja ya umma wa kimataifa - ambao hukabiliwa na hatari kuu ya kudhurika na kuenezwa kwa jangwa kwenye maeneo yao.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA