Hayo aliyasema jana Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2009/2010.
Kapuya amesema kuwa kati ya hao watu wapatao 85,571 wamepata ajira kutoka serikalini, watu 1,185,387 wamepata ajira kutoka sekta binafsi na 965 wamepata ajira kutoka mashirika ya Umma.
Amesema Wizara hiyo imeshatimiza lengo la utekelezaji ya ahadi ya serikali iliyosema kuanzia mwaka 2005 itatoa ajira milioni moja kwa vijana ifikapo mwaka 2010.
Amesema wizara hiyo inaendelea na juhudi za kuhamasisha wizara, taasisi za umma, sekta binafsi na idara kutoa kipaumble kutoa ajira kwa vijana.
Pia amesema wanahakikisha vijana wanapata ajira zikiwemo za kujiajiri kwa kuwa serikali wapo kwenye mchakato wa kuainisha vyama vya akiba na mikopo na manispaa zote Tanzania Bara ambapo zitapewa fedha za mfuko ili wawakopeshe vijana nchini kote.
Vilevile serikali ina mpango kabambe wa kuwawezesha wananchi kiuchumi kuwapatia na kuongeza ajira kwa kuwapa mitaji kwa njia ya mikopo.
0 comments:
Post a Comment