Habari toka dodoma zinasema treni mbili za mizigo zimegongana uso kwa uso asubuhi hii karibu na stesheni ya zuzu nje kidogo nje kidogo ya mji wa Dodoma katika reli ya kati. Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa mkoa, jumla ya majeruhi saba wamefikishwa hospitali kwa matibabu na hadi sasa mmoja ameshalazwa na wengine wanapata vipimo vya x-ray kabla ya kuamuliwa kama walazwe ama waruhusiwe. Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika. Treni moja ilikuw inatoka Dodoma kuelekea Tabora na nyingine ilikuwa inatokea Tabora kuelekea Dodoma. Hii inakuwa ajali nyingine ya tatu katika Mkoa huo katika kipindi kifupi
AJALI YA TRENI DODOMA

0 comments:
Post a Comment