Wednesday, February 22, 2012

MSANII KIDUMU, LINEX, KHADIJA KOPA, SIKINDE NA ‘KINA RIHANNA’ WAKOLEZA MOTO DAR LIVE


Akimshikia maiki mmoja wa wapiga vyombo wake.
Msanii kutoka nchini Burundi, Jean Pierre ‘Kidum’, akikamua  na mmoja wa wasanii wa Bongo, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’, aliyekuwa mshereheshaji wa bonanza hilo. 
Akicheza na mmoja wa mashabiki zake.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Sunday Mangu ‘Linex’, akitumbuiza.
Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Omar Kopa, akiwajibika.
Shabiki akilimaindi jukwaa alipopewa fursa ya kuonyesha machejo.
Msanii mdogo mwenye ‘swagger’ za kiutu uzima,  Hamisi Fadhili aka ‘Dogo Lila’, akiimba kwa mbwembwe.
Walivyowatoa udenda mashabiki.
 Kiongozi wa ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’, Hassan Bichuka, akiwaburudisha mashabiki wake.
 Msaniii akionyesha Ukali Wake
Baadhi ya ‘Kina Rihanna’ walioingia 12 Bora wakiwa katika pozi.
Sehemu ya umati uliofurika kituoni hapo.Picha na Musa Mateja/GPL
---
MOTO mkali uliendelea kuwaka kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala jijini Dar usiku wa kuamkia leo ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo: Linex, Khadija Kopa, Alex Machejo, na makundi ya ngoma za asili ya Machozi na Mawazo Group, bendi ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’, Dogo Lila na msanii Kidum kutoka nchini Burundi, wote hao walikamua sambamba na washiriki wa shindano la ‘Vaa, Imba na Cheza,Kama Rihanna’ na kuufanya umati mkubwa ulifoka hapo kupata burudani isiyopimika katika hali yoyote.
 
Wasanii hao walitumbuiza kwenye Family Day Bonanza ambalo hufanyika kila siku ya Jumapili chini ya usimamizi wa uongozi wa kituo hicho cha Dar Live kilichopo Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaam

0 comments:

Post a Comment