| Mnajimu
na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein
amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar es Salaam. Chanzo chetu cha
habari ndani ya ofisi ya Sheikh Yahya kimesema mtabiri huyo amefariki
dunia wakati akikimbizwa Hospitali ya Ukombozi iliyopo Morocco, jijini.
Sheikh Yahya amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na
aliwahi kwenda India kwa matibabu. |
0 comments:
Post a Comment