TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, May 18, 2010

KWA WALE MNAOWANGIA WENZENU 40 YENU IKIFIKA HUU NDIO MUADHIRIKO WAKE

12:32 AM


Mchawi akijishika kichwa baada ya kupata kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali (Picha na Sufiana Mafoto)

Na Sufianimafoto Reporter, jijini

WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.

Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.

Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”

“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”

Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneohilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukiohilo walisema baada ya kuanguka eneo hilowalimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.

“Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kama hawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema.

“Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ali

Wakazi wa Mbezi Luis, wakimshambulia mchawi huyo.

Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.

Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.

Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilo kutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.


Wakimsindikiza kuelekea katika mtaro ambao walimpiga na bonge la kitofa na kumuua.

3 comments:

Anonymous said...

bt evety1 has the right to life, this isnt justice watanzania wenzangu, tubadilike, whr is the government?

Anonymous said...

I agree with you.....this is totally nonsense. Watanzania, kwa sababu ya njaa na umaskini tunakubalu kurudi kwenye maisha ya karne ya 12 na 13 ya WITCH HUNT bila sababu yoyote.
Huyu jamaa wamemuonea tu, wala hana kosa lolote. Hauna cha uchawi wala nini, hapo ni umaskini tu. Badala ya kupambana na rushwa na viongozi wabovu, wanaanza kugeukiana wenyewe kwa wenyewe.
Uchawi upo bungeni na kwenye baraza la mawaziri katika kutafuta vyeo na madaraka, na sio huko mitaani, ambako kila mtu ananjaa.
Mr. Masue, nyie ndio CIVIL SOCIETY yetu, kwa hiyo tunatarajia muelimishe umma kuhusu haya mambo maovu, badala ya kuyashabikia.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Bwana Masue. Hata mimi naungana na wadau hapo juu. Sidhani kama hali hii ni ya kufanyia ushabiki. Hii ni dalili ya saratani mbaya ambayo tukiendelea kuishabikia namna hii, kuna hatari ya saratani hii kusambaa katika mwili mzima na hatimaye siku moja kutuangamiza. Hebu tuzifanye blogu zetu ziwe chanzo cha mabadiliko tunayoyataka katika jamii yetu! Tazama mtazamo wangu hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/05/fikra-ya-ijumaa-tunasonga-mbele-au.html

Asante!

Post a Comment

 
BONYA HAPA