Katibu mkuu wa TFF FREDRICK MWAKALEBELA kulia , akiwa na kocha wa stars MAXIMO pamoja na mdhamini kutoka SERENGETI TEDDY MAPUNDA.
Kocha MAXIMO amesema kikosi kipo imara kwa ajili ya mchezo huo wa kufuzu fainali za michuano ya CHAN iliyopangwa kufanyika nchini SUDAN ,lakini amesema mazoezi hayakuwa mazuri kutokana na mvua kunyesha bila kukatika.
Amesema licha ya mvua kuharibu mazoezi hayo lakini timu ipo safi kushinda mchezo huo.
Pia amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya mchezo ili kuwahamasisha wachezaji waweze kufanya vizuri katika mchezo huo.
STARS inacheza mchezo wa pili baada ya mchezo wa awali kushinda kwa kuifunga timu ya SOMALIA magoli sita kwa bila katika mchezo uliofanyika uwanja wa UHURU JIJINI DSM.
0 comments:
Post a Comment