TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, February 27, 2010

Waliokamatwa mauaji ya Musoma wafikia 14

10:49 AM
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu, Enos Mfuru.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu, Enos Mfuru, amesema hadi sasa watu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kikatili dhidi ya watu 17 wa ukoo mmoja katika Manispaa ya Musoma, waliokamatwa na polisi wamefikia 14.

Mfuru alisema hayo katika kikao cha ushauri cha mkoa jana na kuongeza kuwa wananchi bado wanaendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za siri kwa jeshi la polisi kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa tukio hilo.

“Napenda kuwaambia tu kwamba, jeshi la polisi kwa kweli limefanya kazi nzuri na ya uhakika. Limewakamata sasa zaidi ya watu 14 tena si kwa kuwasingizia, bali taarifa zinaonyesha walihusika wazi kuwachinja hawa ndugu zetu. Hivyo tuzidi kuwapa moyo polisi ili tufanikiwe kuwakamata wote na kuwafikisha mbele ya sheria,” alisema.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Benedict Mwijarubi, alisema jana kuwa kati ya majeruhi watatu wa tukio hilo, mmoja Moris Mgaya amehamishiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha aliyoyapata. Alisema wengine; Maxmiliani Robert na Maria Kawawa, ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa, hali zao zinaendelea kuimarika.

Alisema wawekezaji, watalii pamoja na wafadhili, wameonyesha nia ya kuusaidia na kuwekeza mkoani hapa, baada ya kuwa wamesusia kufanya hivyo kufuatia mauaji hayo. Mfuru alisema pia watumishi ambao walionyesha nia ya kwenda kufanya kazi katika halmashauri za mkoa, wamekataa nafasi hizo kutokana na matukio hayo ya kinyama yaliyofanyika hivi karibuni.

Aliwaomba viongozi wote wa mkoa wa Mara, wakiwamo wabunge kutumia nafasi zao kuishawishi jamii kuachana na vitendo hivyo, ambavyo alisema vimechafua jina la mkoa. Tukio hilo la mauaji ya kinyama lilitokea usiku wa kuamkia Februari 16 katika mtaa wa Bugaranjabho, Kata ya Buhare ne kidogo ya Manispaa ya Musoma ambapo watu hao wa ukoo mmoja waliuawa kwa kukatwa katwa mapanga na wengine kuchinjwa kama kuku tukio ambalo pia linadaiwa huenda likawa la ulipizaji wa visasi.

CHANZO: NIPASHE


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA