TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, December 11, 2009

Wito wa kuhalalisha ukahaba India

6:54 PM

Mahakama ya juu nchini India imeitaka serikali kutafakari hatua ya kuhalalisha biashara ya ukahaba ikiwa haiwezi kuikomesha.

Mahakama hiyo imesema ikiwa serikali itahalalisha biashara hiyo, makahaba huenda wakarebisha tabia yao huku biashara ya ulanguzi wa wanawake ikizuiwa.

Matamshi ya mahakama yamejiri wakati ikisikiliza kesi kuhusu biashara ya ulanguzi wa watoto iliyofikishwa mahakamani na shirika lisilo la kiserikali.

Ukahaba umepigwa marufuku nchini India lakini biashara hiyo imenawiri katika baadhi ya miji. Kuna takriban makahaba milioni mbili nchini India.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA