TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, December 16, 2009

Wahamiaji Waafrika wakwama Iraq

9:11 PM
Shirika la kimataifa linaloshughulikia maslahi ya wahamiaji, IOM linasema mamia ya wahamiaji kutoka Afrika na Asia wamekwama nchini Iraq.

Wahamiaji hao wanasumbuka kwani hawana fedha za kuwasaidia kuondoka nchini humo.

Msemaji wa shirika hilo Jemini Pandya amesema wanatafuta dola milioni mbili unusu kuwasaidia wahamiaji 700 wanaondelea kuhangaika nchini Iraq.

Amesema kwa miaka sita shirika lake limekuwa likiwasaidia wahamiaji 7,000 lakini ni 32 pekee walioweza kuokolewa mwaka huu.

Ameongeza wahamiaji wengi walihadaiwa kusaini mikataba ya kazi zisiszo za kweli nchini Iraq.

Wengi hupokonywa hati zao za kusafiria na hufanya kazi katika mazingira mabovu.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA