Wakala wa Vipimo na Mizani Tanzania, wamekamata mashine 13 za kuuza mafuta ya petroli Dar es Salaam zilizogundulika kufanyiwa udanganyifu, ili kuwaibia wateja.
Operesheni iliyoendeshwa jana, katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ilibaini mashine hizo katika vituo vitatu, na kuvipiga marufuku kuendesha biashara hiyo.
Kwa mujibu wa mkuu wa operesheni hiyo Wilbroad Kimaro, msako huo umelenga kuhakikisha kuwa watu wanapata huduma zinazolingana na fedha wanayotoa.
Hivi karibuni Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, Ewura, Haruna Masebu, alibainisha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya vituo vyote 900 nchini vinajihusisha na udanganyifu katika biashara hiyo.
0 comments:
Post a Comment