TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, December 12, 2009

Vigogo wapigana vikumbo harusi ya binti Lowassa

4:11 PM

KIKWETE ATIA DOA BAADA YA KUSHINDWA KUTOKEA UKUMBINI, DK SHEIN, MWINYI, KARUME, NAHODHA, DK SALIM, WARIOBA, WATINGA

Ramadhan Semtawa

EDWARD Lowassa, ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu kutokana na kashfa ya mkataba wa kifisadi kati ya kampuni ya Richmond Development (LLC) na Tanesco, juzi alitikisa Jiji la Dar es Salaam baada ya sherehe ya kumuaga bintiye anayeitwa Dk Anna kuvuta vigogo wengi akiwemo makamu wa rais, Dk Ali Mohamed Shein na rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Sherehe hiyo kubwa iliyofanyika Desemba 8 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, ilianza majira ya 12:30 jioni na kumalizika saa 7:30 usiku, lakini Rais Jakaya Kikwete alishindwa kuhudhuria na kutoa udhuru dakika za mwisho.

Wingi wa vigogo hao waliohudhuria sherehe hiyo unaweza kuzidi hata idadi ya vigogo waliohudhuria sherehe za miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kesho yake kwenye Uwanja wa Uhuru.

Wakati mawaziri wa zamani na vigogo wengine hawakuhudhuria sherehe za uhuru, hali ilikuwa tofauti kwenye sherehe ya kumuaga binti Lowassa ambazo zilihudhuriwa na vigogo wengi wa CCM na serikali, ukiacha Rais Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Samuel Sitta na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe.hapa zaidi

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA