TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, December 16, 2009

ruge mutahaba alonga

9:08 PM
JK akiwa na Ruge Mutahaba wakati wa shoo ya THT jijini Dar karibuni
SWALI: Ruge mutahaba ni nani?

RUGE: Nimezaliwa Brooklyn New York Marekani mwaka 1970, Primary School nimesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha nikahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo nilipomaliza darasa la saba. Kisha nikasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo nikarudi Marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University California ambako nikachukua BA in Marketing na pia nikawa nakachukua BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo nikarudi tena Tanzania.

SWALI: Nini kilichotokea hadi ukajikuta uko cloudz FM.

RUGE: Wakati nipo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo tuka-build good friendship. Sasa, niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, Joseph Kusaga akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo nilipojikuta nipo Clouds Entertainment.

SWALI: Tuambie kuhusu THT.
RUGE: Kama Clouds Entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya management ya wasanii ambayo tuliita Smooth Vibes ambayo ndiyo kampuni iliyowatoa wanamuziki kama Lady Jay Dee, Ray C na wengineo. Unajua utakuta kati ya wasanii watano, only mmoja au wawili wana-survive na suddenly utakuta msanii alikuwepo then kapotea. Hii inatokana na kutokuwa na foundation nzuri. Hivyo nikaona ni bora nianzishe House of Talents ambayo sasa kupitia hiyo, tukawa tunawafundisha wasanii misingi ya muziki, kumfundisha msanii how to Manage Industry, Vocal Coaching, Music Business, Music Instrumentation, Dance Classes na kadhalika.
Nikagundua kuwa unakuta msanii anaenda kwenye show lakini performance inakuwa mbovu na pia ili msanii aweze ku-last longer kwenye game anatakiwa ajue dancing. Ndio maana THT tukawa na dance classes. THT imewatoa wasanii wengi kama Maunda Zorro, Mwasiti, Marlaw, Barnaba na wengineo. THT hadi sasa ina miaka minne.

Kupata intavyuu nzima

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA