TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, December 15, 2009

Mwanadiplomasia atimuliwa Tanzania

12:36 PM
Mwanadiplomasia mmoja kutoka Canada aliyemtemea mate polisi na mwandishi wa habari nchini Tanzania anarejeshwa kwao.

Balozi wa Canada Robert Orr aliitwa na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kuzungumiza tukio hilo wiki iliyopita.

Bw Orr alisema, "Kwa faida ya nchi zote mbili, afisa huyo wa Canada ataondoka nchini Tanzania haraka iwezekanavyo."

Hata hivyo, mwandishi wa habari aliyetemewa mate na mwanadiplomasia huyo amesema bado anataka kuchukua hatua za kisheria.

Jerry Muro, anayefanya shirika la habari la taifa la TBC ameliambia gazeti moja la HabariLeo nchini humo , "Haki lazima itendeke. Kumrejesha ni hatua moja tu, lakini haimaanishi kwamba yamekwisha. Nitakwenda polisi kuhakikisha wanashikilia hati yake ya kusafria."

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA