Mazungumzo kwenye mkutano wa kilele juu ya mazingira yameanza tena baada ya matakwa ya nchi changa kuafikiwa.
Mazungumzo ya faragha yataendeshwa kwa njia mbili kama Mataifa makuu yanavyotaka kwa kuzingatia makubaliano ya Kyoto.
Hata hivyo mazungumzo ya kina yanaanza usiku wa leo ingawa bado kuna kazi kubwa endapo makubaliano yoyote yatafikiwa.
Wajumbe wanatafakari maelezo ya mapendekezo mapya yaliyotolewa mapema leo kwenye mkutano.
Kufuatia hatua ya Mataifa machanga kuususia mkutano hapo jana jumatatu ilibidi kufanyike vikao vya ziada usiku kucha ili wajumbe waweze kufidia mda uliopotea.
0 comments:
Post a Comment