
Kilio cha mashabiki wengi wa soka Tanzania kutaka kocha wa timu ya taifa, Marcio Maximo kuachia ngazi, kimezidi baada ya timu ya Tanzania bara kuvurunda katika mashindano ya CECAFA.
Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo iliyomalizika Jumapili mjini Nairobi,Maximo alitamba kwamba angewaziba midomo watu wanaohoji uwezo wake wa kuifundisha timu hiyo kwa kupata mafanikio.
Mashabiki hao wamezidi kufura hasira baada ya timu yao kukosa nafasi za juu, pale ilipojikuta ikishika nafsi ya nne baada ya kuchapwa na ndugu zao wa Zanzibar Heroes goli moja kwa bila.
Baadhi ya wadau wanadai kocha huyo Mbrazil hana jipya katika kuifundisha timu hiyo na kumtaka aachie ngazi.
0 comments:
Post a Comment