
Kanisa katoliki imempokonya upadre askofu wake wa zamani nchini Zambia Emmanuel Milingo kama hatua ya kumzuia kuwatawaza makasisi wanaoishi katika ndoa.
Milingo aliasi maadili ya kanisa katoliki ya maisha ya useja. Makao makuu ya Vatican yamesema hatua yake ni kuhakikisha wanaotawazwa na Milingo hawatambuliwi na kanisa hilo.
Askofu huyo wa zamani alitengwa na kanisa hilo mwaka wa 2006.Msemaji wa Vatican Federico Lombardi amesema Milingo alistahili kufukuzwa, baada ya kuendelea kuwatawaza maaskofu licha ya kutengwa na kanisa hilo.
Aliongeza kutawazwa kwa makasisi wanaoishi katika ndoa ni kinyume na maadili ya imani hiyo na kunatishia kuzua mgawanyiko katika kanisa katoliki.
0 comments:
Post a Comment