TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, August 27, 2009

Wajue Maaskofu Katoliki Tanzania

10:05 PM

Kanisa Katoliki Tanzania lina majimbo ya kiaskofu 31 na maaskofu 32. Kufuatia kifo cha Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Athony Mayalla na jimbo moja kuwa wazi (Same) wanabakia maaskofu 30.

Jimbo Kuu la Dar es Salaam lina Askofu Mkuu ambaye ni Kardinali na Askofu Msaidizi.

Kati ya majimbo hayo 31 kuna majimbo makuu manne ambayo hufanya kazi pia kama ofisi za kanda za majimbo mengine. Majimbo hayo makuu ni Dar es Salaam, Tabora, Songea na Mwanza.

Ifuatayo ni orodha ya majimbo ya Kanisa Katoliki na maaskofu wake kwenye mabano.

Jimbo Kuu la Dar es Salaam (Muadhama Polycarp Kardinali Pengo na Msaidizi wake Askofu, Methodius Kilaini.

Arusha, (Josephat Lebulu), Bukoba, (Nestory Timanywa), Dodoma, (Thaddeus Ruwai’ichi), Geita, (Damian Dallu), Iringa, (Tarcisius Ngalalekumtwa), Kahama, (Ludovic Minde), Kigoma, (Rotas Rugambwa), Mahenge, (Agapitus Ndorobo), Lindi, (Bruno Ngonyani), Mbeya, (Evaristo Chengula), Mbulu, (Beatus Ruwai’ichi), Mbinga, (Emmanuel Mapunda), Morogoro, (Telesphor Mkude), Moshi (Amadeus Msarikie), Mpanda, (Paschal Kikoti), Mtwara, (Gabriel Mmole), Musoma, (Justin Samba) na Mwanza, (Antony Mayalla ambaye amefariki).

Mengine ni Njombe, (Alfred Maluma) Rulenge, (Severin NiweMugizi) Same, (lipo chini ya uangalizi wa padre), Shinyanga, (Aloysius Balina), Singida, (Desiderius Rwona), Songea, (Norbert Mtega), Sumbawanga, (Damian Kyaruzi), Tabora, (Paul Ruzoka), Tanga, (Anthony Banzi), Tunduru/Masasi, (Magnus Mwalunyungu), Zanzibar, (Augustine Shao) na Kayanga, (Almachius Rweyongera)


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA