TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, July 19, 2009

Utapeli mpya wa magari waibuka Dar

3:01 PM
http://media.wheels.topscms.com/images/bf/c6/3033b8df452a863bd86cf2e73b5f.jpeg
Jeshi la Polisi kituo cha Ukonga Sitaki Shari mkoani Ilala, inamsaka mtu mmoja, Joash Jumbura Nyamasagara kwa tuhuma za kutapeli gari aliyoazimwa ili imsaidie wakati wa arusi yake kwa ahadi ya kurudisha baada ya siku nne.

Badala yake, Nyamasagara (pichani) amekaa na gari hiyo kwa zaidi ya wiki tatu sasa hali iliyompa hofu kuu aliyeazimwa na kukimbilia Polisi kuomba msaada wa kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Polisi wanasema katika kipindi cha wiki mbili za awali, Nyamasagara alikuwa anafanya mawasiliano na mwenye gari, lakini wiki moja iliyopita kila anapopigiwa kwa simu yake ya mkononi hapatikani tena.

Kwa mujibu wa habari za kipolisi, kila alipopigiwa simu Nyamasagara alijibu kuwa alikuwa Zanzibar ambako alidai alikuwa akipata fungate, na kwamba wakati wowote angerejea Dar es Salaam.

Polisi wanasema kufuatia kutopatikana tena katika simu yake, mmiliki wa gari hiyo aina ya Mistubishi Galant yenya namba za usajili T 580 BAJ, Yahaya Katanga alilazimika kufikisha shauri hilo kituoni hapo kuomba msaada wa kukamatwa kwa Nyamasagara.

Polisi wa kituo hicho, wamethibitisha kusakwa kwa Nyamasagara kupitia Hati yao namba STK/RB/10143/2009 iliyotolewa kwa mlalamikaji ili imsaidie kumkamata mlalamikaji popote atakapoonekana.

Akisimulia jinsi Nyamasagara alivyofanikiwa kupata gari hiyo, Katanga alisema Juni 24 mwaka huu aliombwa gari na Peter Shirima aliyedai ni rafiki yake mkubwa ili amuazime Nyamasagara afanikishe harusi yake.

Katanga alisema kwa kuwa ameshibana na Shirima, alimpa gari hiyo yenye thamani ya Mamilioni bila woga kwa ahadi ya kurudisha baada ya siku nne.

"Ndipo tukamkabidhi gari baada ya kuandikishiana, lakini baada ya wiki kukatika mimi na Shirima tukawa tunahangaika kumsaka mtu huyo hadi tumefika hapa Polisi," alisema akiwa nje ya kituo hicho.

Aidha, taarifa zaidi za kipolisi zinasema awali Nyamasagara alikuwa akimiliki leseni ya udereva daraja D aliyopata Februari 20, 2000 ambayo ilikoma mwaka 2004, kabla ya kupewa nyingine Februari 20,2007 inayoishia Februari 19 2010.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA