TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, July 31, 2009

Upinzani washangaa kuona Epa bado inatema pesa

2:50 PM

Kambi ya upinzani bungeni imesema imeingiwa na wasiwasi kuhusu hatua ya serikali kutoa dhamana kwa ajili ya malipo kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya shilingi bilioni 65 katika kipindi hiki kinachokaribia uchaguzi mkuu.

Akizungumza kwa niaba ya kiongozi wa kambi hiyo, Hamad Rashid Mohammed, Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Fereji, alisema katika taarifa ya mwaka ya BoT ya 2007/2008 ambayo iliwasilishwa bungeni, imeonekana kuwa serikali ilitoa dhamana ya Epa ya sh. bilioni 65.

Alisema wakati Rais alipohutubia Bunge mwaka 2008 alisema malipo ya Epa yamesimama, lakini serikali bado imetoa ‘special Epa stock’ yenye thamani ya fedha hizo.

“Mara kwa mara serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa malipo ya Epa yamefungwa, vile vile Benki Kuu kupitia kamati mbalimbali za Bunge imesema hivyo hivyo, kumbe hali ni tofauti,” alishangaa.

Alisema kambi ya upinzani inapata mashaka zaidi kwamba malipo haya mapya ya Epa yanafanyika kipindi kinachokaribia uchaguzi mkuu 2010 kwa lengo la kukinufaisha chama tawala kisiasa.

Alisema katika mazingira ya sasa ambapo nchi haina sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha katika kampeni, na kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), hajaanza kukagua vyama vya siasa ili kujua vyanzo vya mapato, ni dhahiri Epa hii maalum ni kiwingu na kwamba kambi ya upinzani inahitaji kupata maelezo ya kinachohusu ‘special Epa stock.’

Akizungumzia azma ya serikali ya kuanzisha upya Mpango wa Kuondoa na Kukuza Uchumi Tanzania (Mkukuta), kambi ya upinzani imeshauri kuwa Mkukuta mpya usianzishwe ili kuondoa mashaka kuwa moja ya chama cha siasa kinatumia Mkukuta kama ilani yake ya uchaguzi na hivyo kuzuia mawazo huru yenye kuweza kuchangia dira ya taifa baada ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwakani.

Kambi hiyo ilishauri kuwa Mkukuta mpya uanze mwaka 2011 na upitishwe na Bunge la Kumi.

Kuhusu mradi mkubwa wa vitambulisho vya taifa, kambi hiyo ilisema imefanya utafiti na kugundua kuwa gharama zinazozungumziwa ni kubwa mno, bila ya sababu, kwani vitambulisho vya aina hii vimewahi kutengenezwa Uholanzi, Afrika Kusini, Nepal na Peru, lakini hata ndani ya nchi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetengeneza vitambulisho 500,000 kwa gharama ya dola za Marekani milioni 3 tu.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA