Mamlaka za nigeria zimeongeza ulinzi kwenye maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kufuatiwa na mapigano yaliyoendelea kwa siku mbili na kuwaacha watu zaidi ya 100 wamekufa. Wanajeshi wameweka vizuizi barabarani katika Mamlaka za nigeria zimeongeza ulinzi kwenye maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kufuatiwa na mapigano yaliyoendelea kwa siku mbili na kuwacha watu zaidi ya 100 wamekufa.
Wanajeshi wameweka vizuizi barabarani katika maeneo yote yaliyoathiriwa na machafuko hayo ikiwemo miji ya Yobe, Kano, Borno na Plateau. Wanamgambo hao wa kiislam walivamia ofisi za polisi na ofisi za serikali.
Kuna taarifa zilizotolewa ya kuwa, kuna makundi ya vijana wenye silaha za mapanga na bunduki wakiiua polisi na raia ovyo.
Majeshi ya Nigeria na Polisi wameamuriwa kutumia kila njia kuhakikisha ulinzai wa nchi hiyo, iliripotiwa na mtangazaji wa shirika la habari la uingerza bi Caroline Duffield kutoka Nigeria.
0 comments:
Post a Comment