TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, July 28, 2009

Serikali yaunda tume kuchunguza ufisadi Tanesco

11:39 PM
Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme Tanesco Dk Idris Rashid ambaye jana wabunge waliibua hoja ya ufisadi(Matumizi mabaya ya fedha za Serikali) unaoendelea kufanywa na shirika lake kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Na Kizitto Noya, Dodoma

SIKU moja baada ya Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa kuibua ufisadi wa Sh1.4 bilioni ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), serikali imeunda tume kuchunguza tuhuma hizo.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliliambia gazeti hili jana kuwa tuhuma hizo ni nzito na hawezi kuacha zikapita bila kuzifanyia kazi.

“Mimi ndiyo kwanza nilizisikia bungeni na kimsingi nilipigwa butwaa, lakini sasa nimeanza kulishughulikia suala hilo kwa kuunda kamati ya uchunguzi,” alisema Ngeleja na kuongeza;

“Ninaamini kazi kubwa, lakini haitakuwa nzito sana kwani mheshimiwa mbunge ametusaidia kwa kutaja namba za nyumba zinazohusika”.

Ngeleja ambaye hakutaja idadi ya wajumbe wanaounda kamati hiyo wala muda watakaotumia kukamilisha kazi hiyo, alisema anaamini uchunguzi huo hautachukua muda mrefu.

Alisema kwa kuwa suala hilo limeibuliwa bungeni, ataweka matokeo ya uchunguzi huo hadharani ili wananchi wajue ukweli wake.

“Of Course (kwa ujumla) tuhuma hizo ni nzito, lakini siwezi kusema lolote zaidi ya kueleza kuwa ninazifanyia uchunguzi. Kazi imeanza leo (jana) na kwa sababu suala hilo limeibuliwa bungeni, tukimaliza kazi tutaijulisha jamii,” alisema Ngeleja.

Juzi jioni wakati akihitimisha mjadala wa wizara yake ya Nishati na Madini, Waziri Ngeleja aliliambia Bunge kuwa tuhuma hizo ni changamoto kwake na kwamba anajipanga kuishughulikia mara moja.

Aliliambia Bunge kuwa anathamini mchango wa mbunge huyo na kwamba isingekuwa rahisi kwake kufahamu jambo hilo kwa kuwa kinachoiunganisha wizara yake na Tanesco ni Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo.

Juzi mbunge wa Sumve Richard Ndassa aliibua ufisadi katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kulieleza Bunge kuwa shirika hilo liko katika harakati ya kuiuza kwa Sh60 milioni nyumba namba 13 iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam, mtaa wa Toure/Chaza line baada ya kuikarabati kwa Sh 600 milioni.

Sambamba na ufisadi huo, pia Shirika hilo linatuhumiwa kutumia Sh1.4 bilioni kukarabati nyumba sita za wakurugenzi kinyume na taratibu.

Ndasa alitoa tuhuma hizo alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa Jumamosi iliyopita na waziri wake William Ngeleja.

Alisema fedha hizo ambazo ni sehemu ya mkopo wa Sh280 bilioni zilizokopwa benki kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo ya Tanesco, imetumika bila ya idhini ya Bodi ya Wakurugenzi.

“Tanesco kuna matatizo makubwa yanayotokana na usimamizi mbovu na matumizi mabaya ya fedha. Shirika halina vipaumbele, linatumia vibaya fedha za umma,” alisema Ndasa na kuongeza:

”Mwaka 2007 shirika hilo lilikopa Sh280 bilioni kutoka benki mbalimbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini badala ya kutekeleza vipaumbele, limeamua kukarabati nyumba za wakubwa kwa Sh 1.4 bilioni," alisema.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA