TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, July 30, 2009

Nigeria; wanajeshi waushambulia msikiti

8:55 PM

Vikosi vya Nigeria vimeushambulia msikiti mmoja ambako wapiganaji wa kundi moja la Kiislamu linalolaumiwa kwa kuzusha ghasia limekuwa likijificha.

Taarifa zinaelezea kwamba wapiganaji wengi wameuawa katika mapigano hayo, ambayo yamefanyika siku ya tatu tangu ghasia kuzuka katika mji wa kaskazini wa Maiduguri.

Wengi ya wapiganaji hao sasa wametoroka, huku wakivishambulia vituo kadha vya polisi.

Kundi hilo la wapiganaji la Kiislamu, linalofahamika kama Boko Haram, linataka kuipindua serikali, na kuanzisha mfumo wa sharia za Kiislamu katika kuiongoza nchi.

Vikosi viliushambulia msikiti huo, baada ya wanajeshi 1,000 zaidi kupelekwa katika mji huo.

Kamanda wa wanajeshi wa nchi kavu, Meja Jenerali Saleh Maina, aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba naibu wa kiongozi wa kundi hilo, aliuawa katika mapigano hayo, usiku wa Jumatano.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA