
Akizungumza baada ya mazungumzo mjini Damascus nchini Syria, mjumbe maalum wa Rais Obama kuhusu Mashariki ya Kati George Mitchell amesema mazungumzo yake na Rais wa Syria yamekuwa ya wazi na matumaini.
Bwana Mitchel amesema mpango wa kuazishwa tena kwa mazungumzo ya amani kati ya Syria na Israeli unakaribia kufikiwa hivi karibuni.
Anatarajiwa kuelekea Israeli katika juhudi za kuanzisha mazungumzo kati ya Israeli na Palestina.
Ziara ya Bwana Mr Mitchell nchini Syria ni ya pili toka mwezi Juni katika juhudi mpya za Marekani kuhimiza amani Mashariki ya Kati toka Rais Obama aingie madarakani mwanzoni mwa mwaka huu.
Ziara hii inafuatia msururu wa ziara kadhaa zilizofanywa na maafisa wa utawala wa Rais Obama nchini Israeli wiki hii, katika kipindi ambacho mahusiano kati ya Marekani na Israeli yakiwa katika mvutano usio wa kawaida.
'Juhudi za kihistoria'
Bwana Mitchell amesema amemwambia rais wa Syria Bashar Assad kwamba Rais Obama amedhamiria kusaidia makubaliano ya kweli ya amani kati ya waarabu na Israeli.
Kwa kawaida katika mahusiano ya kirafiki kati ya pande mbili ni vigumu kukubaliana kila jambo.
''Lengo letu ni kuleta katika eneo hili na watu wake wote fursa ya kuishi kwa amani na heshima. Ili kufanikiwa tutahitaji waarabu pamoja na waisraeli kushirikiana nasi ili kuleta suluhu kamili.
Tunakaribisha ushiriano wa serikali ya jamhuri ya kiarabu ya Syria katika juhudi hii ya kihistoria''. Alisema Bwana Mitchell.
Nao maafisa wa Syria wamesema wametiwa moyo na kile mmjawao amekielezea kama msimamo mpya wa marekani wa kukubali kusikiliza mambo, tangu Rais Obama aingie madarakani mwanzoni mwa mwaka huu.
Damascus ni kiungo muhimu katika ukanda huu kutokana msimamo wake wa kuuunga mkono kundi la wapiganaji la Hamas, kusaidia Hezbollah nchini Lebanon, na pia kutokana na mahusiano yake ya karibu na Iran.
0 comments:
Post a Comment