TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, July 28, 2009

Liyumba: Mambo magumu!

11:49 PM

Mambo yameendelea kuwa magumu katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT, Amatus Liyumba baada ya jaribio la mawakili wa mshtakiwa huyo waliotaka kesi hiyo ifutwe kugonga mwamba leo asubuhi.

Badala yake, kesi hiyo sasa itaanza kuunguruma mbele ya jopo la mahakimu watatu kuanzia Agosti 11, mwaka huu.

Aliyetoa uamuzi huo ni Hakimu Mkazi Eva Nkya, ikia ni baada ya kusikiliza pande mbili za kesi hiyo zilizokuwa zikilumbana vikali mahakamani hapo leo asubuhi.

Upande wa utetezi uliokuwa chini ya wakili Majura Magafu ulitoa hoja ya kutaka kesi hiyo ifutwe kwa sababu siku 60 zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria zimepita bila ya upelelezi kukamilika.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri uliokuwa chini ya Wakili wa Serikali Justine Mulokozi, ulidai kuwa ulikuwa ukifuata taratibu na kwamba sasa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Baada ya kueleza hivyo (kuwa upelelezi umekamilika), wakili Mulokozi akaiomba mahakama kupanga tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Akitoa uamuzi wake, Hakimu Nkya akasema amesikiliza hoja za pande zote mbili na kwamba kutokana na uzito wa kesi hiyo, itabidi isikilizwe mbele ya jopo la mahakimu watatu.

Baada ya hapo, akaiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 11 mwaka huu ambapo mshtakiwa anatarajiwa kusomewa maelezo ya awali.

Liyumba ambaye amerudishwa rumande hadi siku hiyo (Agosti 11), anakabiliwa na kesi ya kutumia vibaya madaraka yake na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi shilingi bilioni 221, katika mradi wa majengo pacha ya benki kuu (BoT).


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA