TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, July 30, 2009

laurence masha mgeni rasmi miss redds kinondoni 2009

11:13 AM
Baadhi ya walimbwende wa redds miss kinondoni 2009 ndani ya mjengoni jioni hii
Moja ya kichwa mahiri kupitia fani ya utangazaji ndani ya Clouds Fm 88.4 alias Mjengoni Kapt Gadner G Habash akizungumza na walimbwende watakaoshiriki kuwania taji la Redds Miss Kinondoni 2009 leo jioni mjengoni hapo Mikocheni,jijini Dar kuhusiana na namna walivyojiandaa kwenye mchuano huo mkali na wa kuvutia.
Aidha shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Boy George Promotions limeweka bayana zawadi mbalimbali watakazozinyakuwa washiriki hao,ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha shilingi milioni moja na laki tano taslim,mshindi wa pili atanyakua kitita cha shilingi milioni Moja,mshindi wa tatu atapata shilingi Laki nane,mshindi wa nne na tano watajinyakulia kiasi cha shilingi laki tatu kila mmoja na waliobaki watapata kifuta jasho cha shilingi laki moja na nusu.
Onesho hilo litakalofanyika siku ya ijumaa pale Mlimani City-Mwenge jijini Dar,kiingilio kimepangwa kuwa ni 10,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu kwa shilingi 40,000/= kwa kila kichwa.Kwa upande wa burudani kundi la Wazee wa Ngwasuma litatoa burudani kambambe kwa wegeni mbalimbali watakaofika katika onesho hilo.
Katika onesho hilo mgeni rasmi atakuw ni Waziri wa mambo ya Ndani Mh.Laurence Masha

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA