KM Ban Ki-moon, kwenye hotuba alioitoa Ulaanbaatar, mji mkuu wa Mongolia Ijumatatu ya leo, kuhusu "Marekibisho ya Kudhibiti Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani" alieleza kwamba nchi zilizozungukwa na bara husumbuliwa sana na vizingiti vinavyokwamisha juhudi za kusukuma mbele maendeleo yao, hususan katika kipindi ambacho nchi hizi zisio na pwani huwa zinaathirika pia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, kijumuisha pia taifa analolizuru la Mongolia, ambapo tatizo la kuenea kwa jangwa huko ni moja ya suala kuu linalozikaba nchi kama hizi kimaendeleo, hali ambayo hunyima umma fursa ya kupata riziki. Uharibifu wa maeneo ya malisho ya wanyama, au machungani, katika Mongolia, aliongeza kusema KM, huathiri sana uchumi wa taifa, na vile vile kuharibu mila na utamaduni wao. Watu wa Mongolia, alitanabahisha KM, ni miongoni mwa watu bilioni 2 ulimwenguni - sawa na thuluthi moja ya umma wa kimataifa - ambao hukabiliwa na hatari kuu ya kudhurika na kuenezwa kwa jangwa kwenye maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment